Tafiti zinaonyesha sababu za wanafunzi kutokuwapo shuleni ni pamoja na utoro, mimba za utotoni, umaskini na mwamko mdogo wa wazazi kuhusu elimu.
Wakati ripoti ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka
2012 , ikionyesha kuwa asilimia 44 ya Watanzania wote ni watoto chini ya
umri wa miaka 15, watoto milioni mbili na nusu wamebainika kukosa
fursa ya kupata elimu ya msingi.
Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Ntambi Bunyazu, anasema kuwa sababu kubwa ya watoto wengi kutokuwapo
shuleni licha ya kuwa na umri wa kwenda shule ni utoro.
“Hata ukiangalia BEST (Kitabu cha Takwimu za Elimu
ya Msingi) ya mwaka 2012 utaona kuwa utoro ulikuwa sababu kubwa ya
watoto kutokuwa shuleni,” anasema.
Anaeleza kuwa, utoro huo unachangiwa na mambo kadhaa, ikiwamo umaskini na baadhi ya wazazi kutokuona umuhimu wa elimu.
Anataja sababu nyingine kuwa ni mimba za utotoni,
ambazo hata hivyo anasema zinachangia sehemu ndogo ya watoto kutokuwa
shuleni.
Kuhusu watoto wasioandikishwa kabisa shuleni,
Bunyazu anasema kuwa hali hiyo inachangiwa na wazazi kutokuona umuhimu
wa elimu kwa watoto wao.
Tatizo la dunia
Siyo Tanzania pekee, tatizo la watoto kukosa fursa
za elimu linaikabili dunia nzima. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki –Moon, hadi kufikia mwaka 2011, takwimu zinaonyesha
watoto milioni 57 hawakuwepo shuleni.
“Watoto milioni 57 hawako shuleni, wanarandaranda
mitaani. Kila ninapotembelea nchi kama vile huko Afrika nimeona watoto
wanarandaranda mitaani au wanacheza, kwa nini wako hapo?’’ anahoji na
kuongeza:
“Wanapaswa wakati huo wawepo shuleni. Hiyo ni
dira yetu, lazima wote tuwarudishe shule. Kila siku watoto 19,000 wenye
umri chini ya miaka mitano wanakufa kutokana na magonjwa yanayozuilika.
Ni lazima tuokoe vifo hivyo vinavyoweza kuepukika.”
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 ya
Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru, Waziri Mkuu Mizengo Pinda
alikiri kuwepo kwa changamoto nyingi katika sekta mbalimbali ikiwamo
elimu.
0 comments:
Post a Comment