Plus 255 Studios

Plus 255 Studios
Home » » Wise Quotes from Mwalimu

Wise Quotes from Mwalimu

Wise Quotes from Mwalimu
Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni"

***********************


'Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana' 01/5/1995
***********************


'Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!' 01/5/1995
***********************


“Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika” –MwalimuNyerere (Januari, 1966)
***********************


"Rushwa ni adui wa haki. Tunamtaka rais ambaye atalitambua hilo na ataichukia rushwa hata ukimuangalia anaonyesha kweli anaiichukia rushwa, sio rais ambaye anayesema kweli rushwa ni adui wa haki....lakini ukimuangalia usoni unashangaa na kusema.... aaaah kweli huyu?
***********************


"Poverty is not the real problem of the modern world. For we have the knowledge and resources which could enable us to overcome poverty. The real problem--the thing which causes misery, wars, and hatred among men--is the division of mankind into rich and poor."
***********************


Not So Sure kama kweli alisema haya na wapi…. lakini inasemekana Source inapatikana kwenye hiki kitabu
Reflections On Leadership in Africa' VUB University Press, 2000.

Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?
***********************


Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii.
***********************


Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga.
***********************


Kukubali kukandamizwa namna hiyo wakati wanayo nguvu inayotokana na wingi wao, ni kwa sababu ni wajinga tu.
***********************


Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache (viongozi) katika nchi yao wenyewe....
***********************


Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao (wananchi) na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili.
***********************


And Not so Wise by Others.., Kwa kweli mpaka sasa siamini kama ni kweli alisema au alisingiziwa

"Kina mama pia endeleeni kuzaa wasichana wazuri kwani katika miaka hii miwili hata kwenye mashindano ya urembo duniani tumetamba." -- Jakaya Kikwete
***********************


Ikiwa tutaruhusu wasichana waliojifungua kurudi mashuleni matiti yao yatakuwa yakichirizika maziwa darasani" --- J.M.Kikwete
***********************


"Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi" J. K. akimtetea mbunge Chitalilo aliyegundulika kuwa kughushi vyeti vya elimu yake.
***********************


"Nafikiri imefika wakati Tuwaombe Rafiki zetu wa Scandinavia,Watufundishe kuandika na Kusoma Mikataba haswa ya MADINI,kwani sie hatuna wataalamu hao" - JK Kikwete May'2007


Nadhani hakuna atakaekataa Hekima zilizojaa katika maneno aliyoyatoa Baba wa Taifa...

Wakuu tukumbushane Wise and Unwise qoutes kutoka kwa viongozi wetu.....

0 comments:

Post a Comment