Bunge la bajeti linaendelea Dodoma Tanzania ( 104.4 CloudsFM ) ambapo
leo May 27 2014 kwenye kipindi cha maswali na majibu asubuhi, moja ya
majibu yaliyotolewa ni kuhusu uwepo wa mbio za mwenge na gharama zake.
Naibu waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Juma Nkamia
amesema ‘serikali kuu hutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji na
gharama halisi ya wakati husika ambapo mwaka 2012 jumla ya shilingi
milioni mia sita hamsini (650) zilitengwa kwa ajili ya kuadhimisha
uzinduzi na kilele cha mbio za mwenge wa uhuru na kati ya hizo milioni
450 zilitumiwa na Wizara na milioni 200 zilitumiwa na mkoa uliokua
mwenyeji wa sherehe za kilele’
‘Kuhusu kiasi cha fedha kinachotumiwa na wilaya, ni kwamba
zinatofautiana kulingana na michango ya Wananchi katika wilaya husika
kwani michango hiyo ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo
huzinduliwa wakati ya mbio za mwenge, kwa ujumla mwaka 2012 Wananchi
walichangia zaidi ya BILIONI 11 na milioni 500′
‘Halmashauri za wilaya na manispaa zilichangia shilingi BILIONI 45,
Wahisani na watu binafsi walichangia zaidi ya shilingi milioni 52 ambapo
faida zinazopatikana kutokana na Mwenge wa Uhuru nchini ni pamoja na
kuendelea kutunza historia na falsafa ya ukombozi wa taifa letu,
kuhamasisha Wananchi kuhusu umuhimu wa kuendelea kuenzi amani,
mshikamano, upendo na zaidi kupambana na ubaguzi wa dini, rangi au
ukabila’
‘Mbio za mwenge wa uhuru hutumika kuhimiza miradi mbalimbali kwa njia
ya kuweka mawe ya msingi au kuzindua miradi iliyowekewa jiwe la msingi
mwaka uliopita na pia kuhamasisha moyo wa Wazalendo na kujitolea kwa
vijana hasa kuonyesha umuhimu na nafasi yao katika kudumisha nchi yao,
kulinda uhuru na kuleta maendeleo ya nchi yao’
Baada ya kusoma haya yaliyosemwa na Naibu waziri wa habari Juma
Nkamia leo May 27 2014 bungeni, unalolote la kuchangia? mtazamo wako kwa
ujumla niachie hapa chini kwenye comment mtu wangu.
Home »
» GHARAMA ZA UENDESHAJI WA MWENGE WA UHURU HIZI HAPA.....
GHARAMA ZA UENDESHAJI WA MWENGE WA UHURU HIZI HAPA.....
Posted by Unknown
Posted on 11:10
with No comments
0 comments:
Post a Comment