Plus 255 Studios

Plus 255 Studios
Home » » HUMPHREY POLEPOLE;UCHAMBUZI WA MWANZO WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA: TUSIKUBALI MASLAHI BINAFSI YASHINDE MASLAHI MAPANA YA TAIFA.

HUMPHREY POLEPOLE;UCHAMBUZI WA MWANZO WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA: TUSIKUBALI MASLAHI BINAFSI YASHINDE MASLAHI MAPANA YA TAIFA.



Nimeisoma Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, nimeisoma yote, ni bahati mbaya inapigiwa upatu kwamba imebeba mambo ya wananchi, mambo ya wakulima, wafugaji, wavuvi, vijana na kadharika. Jamani hayo ni hadaa, msingi wa muundo umebadilishwa, Tanganyika imevalishwa koti jipya la Muungano, ambalo tusipokuwa makini itaendelea kuishi nalo muda mrefu zaidi. Kigezo cha kukataa serikali 3 hakina hoja zenye mashiko, wanasema Hati ya Makubaliano ilisema serikali 2 hivyo hatuwezi badili, huu ni uongo, mbona Hati ilisema mambo ya Muungano ni 11, mbona wao wameweka 14, uhalali wa kubadili mambo ya Muungano kama Hati haibadiliki wanaupata wapi.? Hii ni double standard. hati haikujieleza kwamba kwa baadhi ya maeneo mwiko kubadili na ruksa kwa mengine, Amka ee Mtanzania.

Unasema katika Sura ya Pili unaanzisha Tume ya Mipango ya Taifa ilhali ukijua Zanzibar wana Tume ya Mipango pia, nashangaa sana. Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa inasema Kutakuwa na Dira, Ohoo, kutakuwa tena, nilidhani inapaswa itamkwe, na kwa asili ya "Programmatic Constitutions" Dira inakuwa ni ujumla wa Lengo Kuu la Katiba Pamoja na Malengo Mahususi kama ilivyokuwa kwenye Rasimu..

Wamefuta kumwajibisha Mbunge, wamefuta ukomo, wamefuta mbunge asiwe waziri, wamefanya ugombea binafsi kuwa mgumu zaidi, wamevuruga Tume ya Uhusiano na Uratibu, wao wamesema Tume hii ni kwa Mambo ya Muungano, hili ni kosa kubwa la kisanifu (design), Mambo ya Muungano yanasimamiwa, yasiyo ya Muuungano yanaratibiwa. Wameweka Baraza la Vijana, vijana wenzangu hii ni hadaa, walio wengi ni wanawake mbona lao hawakuliweka, ninazingatia haki hapa, wanataka kuwahamasisha kwa mambo ambayo katika utalaamu na uandishi wa Katiba hayapo, yamewekwa ili msahau yale waliyofuta.

Wamerudisha wakuu wa Mikoa, wananchi mlisema sana juu ya uwepo wa wakuu wa mikoa na wilaya.. kwa namna walivyo rudi sitashangaa wakiendelea kuwa makada wa vyama vya siasa. Haya maoni ya kuwaweka wakuu wa mikoa katika namna hii wameyatoa wapi.? Maoni hayo mimi sikuyaona Tume ya Katiba kipindi chote nilichokuwepo.

Vyanzo vya mapato ni vile vile kwa serikali ya muungano (Katiba ya 1977) na wakadhani mwarobaini ni kurejesha Tume ya Pamoja ya Fedha ambayo haikuwahi kufanyiwa kazi (kuna sababu kubwa zaidi kuliko kuwa na Tume ya Pamoja ya Fedha), Bahati mbaya Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa imelikosa hili.

Rasimu ya Katiba inayopendekezwa inasema Makamu wa Rais Watatu, Makamu wa Kwanza (Muungano), Makamu wa Pili (Rais wa Zanzibar) na Makamu wa Tatu (Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano)... Jamani watanzania wenzangu, huu UTATU mbona tunapewa kwa mgongo wa chupa, TATU tunaziogopea nini.? Tume ya Pamoja ya Fedha iliwaambia anzisheni akaunti ya pamoja ya fedha, ikawa kigugumizi, leo kipi kitafanya tuweze?

Mnasema Mahakama Kuu ya Zanzibar na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano zitakuwa na Mamlaka sawa (concurrent jurisdiction), hata kwa jina hapo si tunadanganyana.? Hakuna kitu kama Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, kwasababu ninyi mnajua haina Mamlaka Zanzibar sasa kuiweka kwenye Muungano kunani.?

NINAENDELEA NA UCHAMBUZI, KAMA NILIVYOSEMA KAZI NDIO KWANZA IMEANZA.

Waraka huu sijauhariri.

0 comments:

Post a Comment