TUKATAE HADAA, SERIKALI YA TANGANYIKA HAIPASWI KUFICHWA KATIKA
SERIKALI YA MUUNGANO NA ZANZIBAR INAPIGWA TEKE PEMBENI, WAISHIO ZANZIBAR
NI WATANZANIA WENZETU. MIMI NINAKATAA HADAA HATA KAMA NIKO PEKE YANGU.
Katiba Inayopendekezwa ya Mhe. Chenge, inatugawa watanzania. Ukiacha
Mbinguni hapa duniani nina Tanzania tu, sitakubali ubaguzi. Katiba ya
Muungano inapaswa kuwa ya Muungano na si ya Tanganyika pekee.
IKUMBUKWE kuwa Vifungu vya Katiba husomwa kwa pamoja, ukiona ulipendalo
limekaa sawa lakini hujali maeneo mengine, wewe huna tofauti na
wabinafsi wale wale. Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa UBORA wake ni
UJUMLA wake.
1. Vijana
mkifurahia Baraza la Vijana ndani ya Katiba ilhali Muundo ni mbaya na
mnajua Baraza hilo ni kwa Tanganyika pekee, huo ni ubinafsi, mmewatenga
vijana wenzenu wa Zanzibar. Na mkumbuke changamoto za vijana
hazitaondolewa na Baraza la vijana. Jiulizeni kama Katiba hii ni ya
wananchi, mbona Baraza la Wanawake hakuna maana wenye shida zaidi ni
wanawake na ndio wengi kwa idadi, mbona Baraza la NGOs halijawekwa. Mimi
ni kijana na sikubali kuhadaiwa, Mambo hayo sio ya Muungano na
hayapaswi kuwa katika Katiba ya Muungano.
2. Wakina mama zangu
msifurahie 50/50 mkaridhika ilhali mkijua muundo wa Bunge la Muungano
una matatizo, wakati mkijua fika hayo mambo ya wanawake hayatekelezwi
kimuungano, je mmekuwa wabinafsi kiasi hiki kwamba wanawake wenzenu wa
Zanzibar hamuwajali. Ama ndio shida yenu ikionekana kuanza kuondoka
shida ya wenzako si yako? Tafakarini wamama na dada zangu, katika hili
tuko pamoja. Tusiwapongeze ilhali tunajua dhamira yao si safi.
3.
Wasanii wa tasnia mbali mbali ni kweli kazi yenu imeisha? La hasha.
Katiba ni kama mwili wa Binadamu, Mwili umekuwa unaumwa kwa muda mrefu,
sasa tunaupatia tiba kwa ujumla wake, hivi mdogo na masikio ukionekana
kuelekea kupona utapuuza maumivu ya kichwa, miguu, mikono, macho,
mgongo, tumbo na sehemu nyingine za mwili? tena la hasha, mambo ya
wasanii hata leo hayatendewi kimuungano, mbona hatuwahoji akina Mhe.
Sitta na Chenge, kwanini tunaweka mambo ya Tanzania Bara katika Katiba
ya Muungano na tunayaita ya wananchi wa Tanzania. Hatutakuwa tumepona
kama tutaridhika kwetu kuna amani na kwa jirani kunawaka moto. Mimi ni
msanii, ni mchoraji na nimesoma uchoraji kwa miaka 10, mimi ninapiga
gitaa na ninapenda kuimba, ila nakataa hadaa.
4. Wakulima ninyi
ndio mnasukuma kwa kiasi kikubwa gurudumu la uchumi wa Nchi yetu.
Wanasema wameweka mambo ya wakulima sawa. Niwaambize mama, baba, dada,
kaka, rafiki na ndugu zangu, Kilimo sio jambo la Muungano tangu tuungane
mwaka 1964. Iweje leo wawaambie mambo yenu yapo katika Katiba ya
Muungano wakati kiutendaji ni kwa watanganyika pekee. Sidhani kama
wakulima ni wabinafsi kwamba maadamu mambo ya wakulima wa tanzania bara
wamekaa sawa, mtapuuza wakulima wa mwani, karafuu na mpunga kule
Zanzibar.
NINAENDELEA
..............haija haririwa............
0 comments:
Post a Comment