Baada
ya kuwafahamu majaji wawili wa TPF6 ambao ni Ian Mbugua (Kenya) na
Juliana Kanyomozi (Uganda),
hatimaye jina la jaji wa tatu limefahamika
ambapo C.E.O wa BHitz Music, Hermes Bariki a.k.a Hermy B (Tanzania)
ndiye atakayeungana na majaji hao wawili.
Akiongea
na 100.5 Times fm Hermy B amewashauri watanzania kuwasapoti washiriki
wanne kutoka Tanzania kwa kuwapigia kura kwa kuwa ushindi hutokana na
wingi wa kura anazopigiwa mshiriki na sio anachosema jaji.
“Watanzania
wasifikirie kwamba Jaji wao ndiye atakayewapatia ushindi washiriki
wao, ndio wapige kura sasa, kwa sababu ushindi wa watu wengi unatokana
na kura na sio jaji, hata Juliana akimwambia you are the best of the
best lakini asipopigiwa kura hawezi kushinda.” Amesema Hermy B.
Washiriki watakaoiwakilisha Tanzania katika TPF6 ni Angella Karashani a.k.a Angel, Tanah, Hisia na Dubson.
Mshindi
wa mwaka huu atapewa shilling Million Mia Moja, na mkataba wa kurekodi
nyimbo kwa gharama ya shilingi Million mia mbili za Tanzania.
0 comments:
Post a Comment