Home »
» Exclusive VIDEO: Makada wa CCM na ACT-Tanzania watajwa kuihujumu CHADEMA!
Exclusive VIDEO: Makada wa CCM na ACT-Tanzania watajwa kuihujumu CHADEMA!
Posted by Unknown
Posted on 10:15
with No comments
Mwanasheria mkuu wa Chama Tundu Lissu anaingia na Madiwani wetu wa Shinyanga hapa
Diwani Sebastiani amewaambia wanahabari kuwa mwakajana walifanya vitendo haramu wakishirikiana na CCM na baadhi ya waliokua wanachadema wakiongozwa na Mchange. Wanasema wamekuja kuomba toba kwa viongozi wa juu wa CHADEMA na wanachama ili wasamehewe kwa usaliti huu mkuu
Wanasema baada ya Zitto kuvuliwa madaraka ndani ya Chadema ,Mchange alipewa Dili na CCM la kuwarubuni madiwani na viongozi ndani ya CHADEMA ili watoe matamko na kuonyesha kuwa Chama kina mpasuko
Anasema January 2014 Mchange alimpigia simu kuwa Naibu waziri wa Nishati na Madini Steven Masele ana dili la shilingi milioni 180. Na baadae Masele alimpigia simu wakakutana na kupanga njama za kufuatilia ziara ya Dr. Slaa kanda ya ziwa na kupanga kuilipua Helkopta ya Dr.Slaa iliyokua itue Shinyanga .
Anasema alijiandaa na kufuatilia ila hofu kubwa ya kimungu ikamuingia akahofia taifa litapokeaje tukio la kifo cha Dr.Slaa na yeye kuhusishwa?
Pia alikutana na Nape Nnauye aliyepanda ndege kutoka Dar Es Salaam na akamueleza kuwa alisikitika sana kuvuliwa madaraka kwa naibu katibu mkuu CHADEMA Zitto Kabwe.Walikutana hotel ya Kalena -Shinyanga Mjini
Baadae alitafakari sana akashauri watumie mabango na kurubuni vijana angalo kuhujumu ziara ya Dr.Slaa
Baada ya kufanikisha Zoezi hilo Walikutana tena na Nape kisha Mwigulu Nchemba akawaomba wawashawishi madiwani na viongozi wengine wahamie CCM kwa Ahadi ya kupewa ukatibu wa Wilaya kwenye wilaya watakazoamua
Wakati wa Uchaguzi wa Kalenga waliitwa Dodoma wakakutana na Kinana Nyumbani kwake na aliwapongeza kwa uamuzi wao na pia akawaahidi kuwa atawapa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha wanaboresha mgogoro uliopo CHADEMA na pia akawaahidi watagharamia pesa za kwenda mikoani na pia wakasema kuna chama kitasajiliwa kitaitwa ACT na watahakikisha msajili anawapatia usajili na kuwa hiyo itakua mbinu kali ya ushindi
Pia alisema watahakikisha Wabunge wanne wa CHADEMA hawarudi Bungeni na ACT itasaidia kutoa mgombea hasa kwa jimbo la Tundu Lissu ambaye atafadhiliwa ili kugawa kura za jimbo. Akasema, Lema, Msigwa na Mbilinyi wataandaliwa mkakati Maalumu na muda ukifika watautekeleza na watashirikishwa.
Wanasema kadiri CHADEMA ilivyokua ikizidi kupata Unaarufu wakaanza kujiskia vibaya huku CCM wakishindwa kutimiza ahadi zao kwao.
Wakaanza kujadiliana wao kwa wao kisha wakaamua watubu,warudi waombe radhi kwa viongozi na wanachama kwa usaliti huu .
Wanaomba chama kiwapokee na wapewe fursa nyingine.Dhamira zao ni nzito sana.Wanamuomba Mungu awape moyo mwepesi wa kusamehe kwa kitendo hiki cha kishetani walichofanya.Wanaomba Mungu aibariki CHADEMA,Mungu aibariki Tanzania
Mratibu wa Kanda ya Ziwa Mashariki : Anasema Kanda ya Ziwa Mashariki wamewasamehe hawa madiwani lakini madiwani wakaomba nafasi ya kuongea na viongozi wa ngazi ya Taifa ili waombe radhi kwa wanachama wa Chadema nchi nzima na wapenda mabadiliko
Tundu Lissu Sasa
Tundu Lissu: Anasema Madiwani hawa kwa taarifa zilizopo kwa vyombo vya habari walitangaza kujivua uanachama na udiwani wao. Anasema kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa,Diwani akijiuzulu anatakiwa aandike barua rasmi kwa mwenyekiti wa Halmashauri na kuambatanisha na kiapo .Hawa hawakufanya hivyo kwa hiyo bado ni madiwani wa halmashauri ya mji wa Shinyanga
Na uthibitisho kuwa hawajajiuzulu ni kuwa siku 90 zimepita bila kutangazwa uchaguzi
Anaendelea kusema Habibu Mchange ukiachilia mbali amewahi kufukuzwa CHADEMA,ukifuatilia utakuta yeye Juliana Shonza na Mtela Mwampamba ndio wamekua wakiandaa mikutano kabla na baada ya Zitto kufukuzwa.Pia amehusishwa na kampuni iliyofanya uhalifu ya Gombe advisors na Lekadutigite. Anasema Lekadutigite ilipewa milioni 120 na NSSF miezi mitatu baada ya Zitto kufukuzwa ambaye ni mmoja wa wanahisa wa kampuni hizo
Sasa Zitto ambaye ni Mwenyekiti wa Hesabu za Mashirika ya Umma anapewa fedha na NSSF Leo anasema Bungeni hataki Posho kwa sababu huko anakopewa milioni 120 kwa miezi 3 kunamuwezesha
Anasema sasa tujifunze kuunganisha dots kuhusu watu wote hao waliotajwa
Lissu anaendelea kusema, kuna sheria ya kupambana na ugaidi. Watu wanakula njama za kulipua ndege na kuua nahasimu wao wa kisiasa. Anasema huu ni Ugaidi. Hakuna jina lingine. Sasa anaitaka mamlaka husika zichukue hatua za wazi kuanzia uchunguzi ili wahusika washughulikiwe haraka kwa mujibu wa Sheria. CHADEMA tumefanyiwa njama hizi na sasa tumechoka. Tukio la Arusha na mikoa mingine tumeshambuliwa na pia wanachama na viongozi wetu wamenusurika kuuawa na wengine wameuawa.
Anasema hayo ya kupanga njama ovu za kisiasa kuwang'oa majimboni hakuna shida na wanawakaribisha nyumbani
Amemaliza anapokea maswali.
Akijibu swali la Waandishi wa Habari anasema wabunge wetu wanaohudhuria Bungeni wanakiuka azimio la kamati kuu.Na kama mnavyojua kamati kuu yetu yetu haichezewi, hailei mayuda iskarioti. Haijawahi kuogopa na haimuogopi Leticia Nyerere,Shibuda au Said Arfi. Ni bora wawe wabunge wa mahakama kama jamaa yao. Watatueleza wakati utakapofika
Asanteni sana!
0 comments:
Post a Comment