Plus 255 Studios

Plus 255 Studios
Home » » HII DHANA YA UBAGUZI NI DHAIFU, FUATILIA TAFAKURI YANGU HAPA

HII DHANA YA UBAGUZI NI DHAIFU, FUATILIA TAFAKURI YANGU HAPA


Nimefuatilia kwa ukaribu kituo kimoja cha Televisheni ambacho kimekuwa kikitumia dhana ya “ubaguzi” ku-dismiss Pendekezo la Serikali 3 na kujenga Hoja ya Serikali 2. Hii ni dhambi kubwa na ndiyo aliyokuwa akiikemea Mwalimu Nyerere. Hoja ya Serikali 2 haijengwi kwa kushambulia pendekezo la Serikali 3, Kamwe Aslan.! Kizuri chajiuza

Huwezi kwenda kila kona na kuhoji hoji wazanzibari waishio Bara juu ya umuhimu wa Muungano ili ku-justify kwamba Zanzibar inaihitaji Tanganyika zaidi, hii ni victimization, ni unyanyasaji, ni kupanda mbegu ya ubaguzi, kiukweli sote tunahitajiana.

Na nijikite tena katika kueleza ukweli kwamba Rasimu inaondoa kabisa ubaguzi wa wa aina yoyote katika Jamhuri ya Muungano, kwa lugha rahisi neno ubaguzi pamoja na Ibara ya 25 juu ya “Marufuku kuhusu Ubaguzi” limetajwa mara 14 katika Rasimu ya Pili. Tazama pia Ibara ya 25(5) inayotoa tafsiri ya neno “Ubaguzi”.

Rasimu inajali Raia ambao kwa ujumla wao wanaishi Tanzania Bara na Tanzania-Zanzibar/“Zanzibar”,Ibara ya 29 inasema kila Raia ana uhuru wa kwenda kokote na kuishi katika Jamhuri akitaka, sasa ubaguzi uko wapi.?

Hakuna Raia wa Tanganyika au Raia wa Zanzibar, na zaidi ni kwamba Tanganyika na Zanzibar ni “maeneo tu” au “sehemu tu” ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sema Rasimu ya Pili katika kutambua nafasi yao katika Muungano tumezipa hadhi ya utambulisho kwamba Tanganyika na Zanzibar ni “Nchi Washirika” kama inavyojipambanua katika Ibara ya 64(1).

Ikumbukwe hata Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar hazitafanya mambo yao kiholela bali kwa kuzingatia Katiba hii “kwanza” na kasha Katiba zao, hili liko bayana katika Ibara ya 64(4), zingatia pia Ukuu wa Katiba katika Ibara ya 8.

Sasa hawa wanaosema Rasimu ina chembe za ubaguzi hayo wanayoyasema wameyatoa wapi.? Hao wanaosema wapemba walio Bara watafukuzwa wameyatoa wapi.?

Hasa vijana wenzangu, Nchi hii ni yetu leo na kesho, tukiwa wanafiki hatujitendei haki leo na hata hatulitendei haki Taifa letu leo na kesho. Jiulize unatetea jambo Fulani kwa sababu zipi.? Ni msimamo wako kweli au unajaribu kuwafurahisha watu.?

Hizi akili za kuambiwa jamani naomba mchanganye na za kwenu.

Angalizo: Andiko huenda limetumia lugha nzito kwa baadhi ya maneno, niwatake radhi, ilikuwa katika kushajihisha hoja.

# source; Humphrey pole pole

0 comments:

Post a Comment